HATUA YA KWANZA:-
〰️ Kubali na Amini kuwa
umempenda ila yeye hajakupenda kama ulivyompenda wewe.
Kubali uhalisia
kuwa hupendwi au umeachwa. Ikiwa
hutokubali kuwa
umeachwa, umependa Ila hupendwi utajikuta unawekeza nguvu zako nyingi katika
kujenga mahusiano yanayokuumiza kila kukicha.
HATUA YA PILI:-
〰️ Chukua wakati wako kwa ajili ya kuondoa uchungu uliopo
moyoni mwako kwa kulia au kuhuzunika. Hali hii itaondoa hasira na chuki za
maumivu ya mahusiano yako.
HATUA YA TATU:-
〰️ Jifunze kuwa busy kwa
kufanya kazi napia tenga mda wa kufanya mazoezi ya mwili. Hatua hii
itakuwezesha kuondoa maamivu yako na kumsahau yule aliyekuumiza kwa kadri
unavyokuwa busy na shughuli zako za maisha yako ya kila siku. Zingatia, maumivu
yako hayawezi kuondoka ikiwa hutokuwa na kitu kinachokufanya uwe busy, kitu
kinachochukua umakini wako...
HATUA YA NNE:
〰️ Msamehe mtu huyo kwa
kukuvunja moyo katika Mahusiano, lakini usijaribu au kufikiri na kumpa nafasi
ya kumwamini tena. Jifunze kumwepuka kadri uwezavyo ikiwa ni mtu ambaye mpo nae
karibu, iwe ni kazini au sehemu mnayoishi.
HATUA YA TANO:-
〰️ Ondoa karibu
yako vitu vyote vinavyowezekana vya mtu huyo ulivyonavyo, Mfano zawadi
alizowahi kukupatia au Kumbukumbu za matukio ya picha zote ulizowahi kupiga
nae. Vitu vya mtu ulivyonavyo huambatana na nafsi yake, kuendelea kuvihifadhi
vitakufanya ushindwe kumsahau katika maisha yako wakati yeye hana mpango na
wewe kabisa...
HATUA YA SITA:-
〰️ Tengeneza wakati
wako wa furaha. Jitengenezee kumbukumbu nzuri kwa kutumia mda wako mwingi na
marafiki zako au wa watu wanaokuthamini.
HATUA YA SABA:-
〰️ Shukuru kwa yote
yaliyopitia hata kama yamekuumiza kiasi gani, Amini kuwa hakuwa chaguo lako,
unaweza kuanza upya na unaweza kuishi maisha yako bila yeye.....
USISAHAU....
Kwa Imani yako uliyonayo, Ikiwa mwanzo hukuzungumza na MUNGU kwa kuyaombea
mahusiano yako, tumia mda huu sasa kumwomba MUNGU akuonyeshe mtu sahihi mwenye
kufanana na wewe Kama yasemavyo Maandiko....
Imeandaliwa na;-
Mwanasaikolojia & Mshauri nasihi,
Eng GADAFI NGUILE 💭
№ +255745228862 (WhatsApp)....
No comments:
Post a Comment