Kijana au binti wa leo je hupo kwenye kipindi cha kumtafuta mke mwema au Mme mwema? Karibu nikujuze kitu hapa ambacho kitakusaidia kwenye maisha yako yote hapa ulimwenguni
*➡Kiufupi ni hivi kidini neno mchumba limejitokeza mala chache sana tena katika baazi ya biblia na Quran
lakini katika vitabu vingi vya kidini neno mchumba halipo kabisa isipokuwa
neno linaloonekana sana ni "MKE"*
Wakati nalifuatilia neno hili mchumba kibiblia nilijiuliza maswali kadhaa
ambayo ni;
*1.Kwanini neno mchumba halijatumika sana kibiblia?*
*2.Je waandishi wa biblia
kuna makosa ya kiuandishi waliyafanya kiasi cha kushindwa kuliandika neno
mchumba kwa sana?*
*3.Kwanini neno mke likatumika sana kuliko neno mchumba?*
Haya maswali yalinifanya nijiulize sana baadaye nikapata hekima ya kimungu juu
ya suala hili
NI HIVI SABABU KUBWA YA VITABU VYA MUNGU KUTUMIA NENO MKE KULIKO MCHUMBA NI
KWASABABU.
"KUSUDI LA MUNGU LA KUMKUTANISHA MTU MKE NA MTU MME NI ILI
WAWE MWILI MMOJA YAANI MKE NA MME NA SI WAWILI TENA"
*👉Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na
mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.*
Kwahiyo kitendo cha binti na kijana kukubaliana kwamba wapo tayari kuwa mke na
Mme kiroho wanakuwa si wawili tena bali mtu mmoja unajua kilichowaunganisha
hawa ni nini? ni maneno au kiapo kilichowafanya wawe na mwelekeo mmoja
Nachotaka uone hapa ni neno linalosema *👉"ahadi yako kwa mke wa ujana wako"*
Kwahiyo utaona yakuwa kijana na binti wanapoanza kupeana ahadi na wakakubariana
basi kibiblia hata kama bado hawajaidhinishwa madhabahuni tayari wanakuwa ni
mke na mme kwa jinsi ya kiroho si wachumba
*ANGALIZO*
➡Kuwa mke na Mme kiroho
haiwapi uharali wa kuishi nyumba moja wala kufanya mapenzi bali ni mpaka pale
mtakapoidhinishwa na Shekh au madhabahuni
➡Kijana unayependa
kuchumbia binti zaidi ya mmoja na wote unaishi nao umejifunga mwenyewe kwa
viapo vyako kwa jinsi ya kiroho so kuwa makini sana
Baada ya kukuelezea kwa ufupi Kwanini vitabu vya mungu vimetumia neno mke sana
kuliko mchumba twende kuona jinsi binti au kijana anavyoweza kumjua Mme au mke
mwema atokaye kwa Bwana
*◾Anayefaa kuwa mke au mme
wa fulani anakuwa na tabia za mke au Mme hata kabla hajaoa au kuolewa*
➡Binti anayefaa kuwa mke
wa fulani anakuwa na tabia kama za mke wa fulani kabla hata hajaolewa!
*✍Mke wa mtu hauwezi
ukamkuta amevaa ovyo au amevaa nguo zinazoweka maungo yake nje atajipamba
vizuri kwa mavazi ya adabu ni hivyo pia binti anayefaa kuwa mke wa fulani
atavaa vizuri maana anajua mwili wake ni hekalu la Roho mtakatifu na ni fahari
ya mmewe*
*✍Mke wa mtu hauwezi
ukamkuta bar akinywa pombe ni hivyo pia binti anayefaa kuwa mke hauwezi kumkuta
bar*
*✍Mke wa mtu hauwezi
kumkuta anaongea ovyo bila adabu mitaani au kwenye daladala ni hivyo pia binti
anayefaa kuwa mke hauwezi kumkuta akiongea ovyo bila adabu*
*✍Mke wa mtu hauwezi
kumkuta uchochoroni usiku wa manane ni hivyo pia binti anayefaa kuwa mke
hauwezi kumkuta uchochoroni usiku wa manane*
*✍Mke wa mtu hauwezi
kumkuta kwenye mitandao akiwa ameposti picha za uchi ni hivyo pia binti
anayefaa kuwa mke hauwezi kumkuta kwenye mitandao akiwa ameposti picha za uchi*
Kwahiyo kijana kama unamhitaji mke mwema utaziona tabia za mke mwema kwa binti
hata kabla hajawa mke wa mtu
Kwako binti👇
*➡Binti na wewe
unayemhitaji Mme atokaye kwa Bwana utamjua kijana kwa tabia zake za Mme hata
kabla hajawa Mme wa Fulani*
✍Mme wa mtu hawezi
kushinda kijiweni asubuhi mpaka jioni bila kazi yoyote ni hivyo pia kijana
anayefaa kuwa Mme hauwezi kumkuta kijiweni bila kazi yoyote
✍Mme wa mtu hawezi kukosa
adabu kwa watu waliomzidi umri ni hivyo pia kijana anayefaa kuwa Mme wa mtu
hawezi kukosa adabu mbele za watu waliomzidi umri
✍Mme wa mtu hawezi kuwa na
sifa ya uzinifu katika jamii ni hivyo pia kijana anayefaa kuwa Mme wa mtu
hauwezi kumkuta ana sifa ya uzinzi katika jamii iliyomzunguka
✍Mme wa mtu hauwezi kumkuta hana uwezo wa kuihudumia familia yake mwenyewe ni hivyo pia kijana anayefaa kuwa Mme wa mtu hauwezi kumkuta hana uwezo wa kujihudumia mwenyewe Bali Mara nyingi utamkuta ana focus sana na maisha yake ya baadaye na pia ana nidhamu ya maisha.
➡Na pia haauwezi kumkuta
kijana anayefaa kuwa Mme wa mtu👇
*-Ana matumizi ya ovyo ya Pesa maana anaihofia kesho*
*-Hauwezi kumkuta anafanya maamuzi ya kitoto kwenye mambo mhimu yanayomhusu*
*-Na pia hauwezi kumkuta anaishi kihasara hasara
➡Badala yake utamkuta
*-Ni mtu mwenye misimamo na maisha*
*-Nadhifu*
*-Mtanashati*
*-Smart kichwani*
*-Mcha Mungu*
*-Na anayejua kuongea kwa hekima na busara mbele za watu*
*◾Kwahiyo kijana anayefaa
kuwa Mme wako binti utamkuta ana tabia zinazofananana kama za mme wa mtu kabla
hajaoa au hajakuoa*
Yapo mengi nilitamani niseme lakini sitaki nikuchoshe ila haya machache
yanaweza kukuhekimisha binti au kijana unayetafuta mke au Mme mwema atokaye kwa
mungu
Mungu awabariki sana🙏
WhatsApp 0745228862
Eng GADAFI NGUILE
No comments:
Post a Comment