Monday, August 25, 2025

POLISI WAKAMATA SHEHENA LA NYAYA ZA SHABA ZA KAMPUNI YA TENESCO-MKURANGA-PWANI

Jeshi la Polisi Mkoa wa pwani ,Wilaya ya Mkuranga katika Mkoa wa kipolisi Rufijj limewakamata Watu wanne kwa vipindi tofauti wakidaiwa kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Shirika la Reli Tanzania (TRC).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkoa wa Kipolisi Rufiji, watuhumiwa wawili walikamatwa Desemba 13, 2024 wakiwa na vipande vya shaba 426 vyenye uzito wa kilo 7,728 na nyaya za shaba zenye uzito wa kilo 2,628.5 zilizotambuliwa kuwa ni mali zilizoibwa kutoka kwenye miundombinu ya Tanesco.



Pia wanadaiwa kukamatwa na nyaya za shaba za TRC zenye uzito wa kilo 430 na vipande vya shaba vilivyotengenezwa kutoka kwenye nyaya ambaz0 zimeibiwa Tanesco na TRC ili kuficha uhalisia wake.
Mara kadhaa TRC imekuwa ikieleza kuwapo kwa baadhi ya watu wanaokula njama za kuharibu miundombinu ili kuzorotesha usafiri wa treni ya kisasa (SGR).





No comments:

Post a Comment

POLISI WAKAMATA SHEHENA LA NYAYA ZA SHABA ZA KAMPUNI YA TENESCO-MKURANGA-PWANI

Jeshi la Polisi Mkoa wa pwani ,Wilaya ya Mkuranga katika Mkoa wa kipolisi Rufijj limewakamata Watu wanne kwa vipindi tofauti wakidaiwa kuhuj...