JESSICA COX ni mwanamke mmarekani aliyezaliwa mnano mwaka 1983 bila mikono lakini ndiye mwanamke pekee wa kwanza asiye na mikono pekee duniani kupewa leseni ya kurusha ndege.
Mwanamke rubani asiye na mikono hivyo anaongoza ndege kwa kutumia miguu yake!
Na huu ndio upekee wake mkubwa kwa marubani wote duniani ukiangalia kwa hali ya
kawaida hana viungo ambavyo ni mikono inayotumika kuongozea ndege lakini kwake
kutumia miguu ndicho kimekua kitu chake cha pekee sana na kujitofautisha sana
rubani yoyote Duniani na ndicho kinaishangaza dunia kutoka kwake!
Katika kitabu chake cha "Disarm your Limits" moja ya msemo
wake anasema katika maisha huitaji kuwa na mikono ili uwainue watu kutoka chini
ila unahitaji moyo wa Upendo wa kudhati kuwatia moyo na kuwaonesha wanaweza
kufanya nakubwa haijalishi walivyo haikua rahisi kwangu kuthubutu kufanya
ninachofanya, haikua rahisi nikijiona nilivyo na maamuzi ya kujifunza urubani!
Anasema haijalishi ulivyo na watu wanakuonaje unahitaji mambo muhimu sana kama.
Kujiamini mwenyewe hata kama wengine hawakuamini, haikua rahisi watu kuamini
kama nitaweza kuongoza ndege bila mikono sasa naongoza, unahitaji uvumilivu
mkubwa, unahitaji kujaribu Mara mia Mara elfu mpaka uweze, unahitaji kushindwa
Mara nyingi ili ushinde, unahitaji kushinda roho ya uoga na anasema vikwazo
vingi vinavyotuzuia ni kwa sababu ya mtazamo wetu hua tunavitengeneza wenyewe
kiuhalisia havipo!
Amini wewe ni mashindi hata kama hakuna anayeamini wewe ni mshindi kwa sababu
ya muonekano wako wa nje lakini jiamini na jikubali mwenyewe jinsi ulivyo
ushindi uko ndani yako!.
Jifunze jambo kutoka kwa Jessica cox rubani asiye na mikono!
Kitu ambacho kinaonekana ni udhaifu wako hicho kinaweza kuwa fursa ya
kuishangaza dunia na ndicho kinaweza beba tofauti yako na THAMANI yako!
USIKATE TAMAA JINSI ULIVYO UNAWEZA UNA UKUU NDANI YAKO!
Kama umependa makala hii tafadhali share na wengine.
See You At The Top
NO:
+255745228862 WhatsApp (Gadafi Nguile)
Eng Gadafi Nguile
No comments:
Post a Comment