Kila mwanadamu mungu kampa kile anacho stahili nikiwa na maana ya kwamba kila mtu ana kipaji chake ambacho kapewa na mungu lakini ndani ya hicho kibaji kuna nguzo mahususi ambazo kati ya hizo nitazitaja 5 kwa njia ya maswali ambazo ni;
i. Jua Kipaji Chako Kimebeba THAMANI Gani?
ii. Kipaji Chako Kinalindwa Namna Gani?
iii. Kipaji chako ni kwa ajili ya watu gani?
iv. Kipaji Chako Kinajitofautishaje?
v. Kipaji chako Kimeambatana na Hatari Gani?
Katika Makala Hii Tutazungumzia Nguzo ya Pili?
- Kipaji Chako Kinalindwa Namna Gani?
Kila kipaji lazima kilindwe ili kiweze kuwa na ufanisi na kitoe matokeo makubwa
na pia kiishi kwa muda mrefu zaidi.
Kama unataka kufanikiwa kukifanya kipaji chako kizalishe thamani ya kifedha ni
lazima ujue mambo yanayohitajika kufanyika ili kukilinda.
Kuna watu ambao waliwahi kuibuka wakiwa na vipaji vikubwa sana ila hawakuweza
kudumu kwa muda mrefu kwa sababu walishindwa kuvilinda vipaji vyao.
Ukiwa na kipaji ila ukashindwa kukilinda basi kinaweza kisikupe faida ama
kikakupa faida ya muda mfupi sana.
Kwenye kulinda kipaji chako ni lazima ujue kuhusu “Do’s and Don’t’s” (Mambo
unayopaswa kuyafanya na yale usiyopaswa kuyafanya).
Kubeba kipaji chako na kukifanya kilete matunda hakuna tofauti kabisa na mama
ambaye ni mjamzito, kuna masharti anatakiwa ayafuate sio kwa sababu yake yeye
ila kwa sababu ya usalama wa mtoto aliyeko tumboni kwake.
Kuna mambo lazima ujizuie kuyafanya na mengine ujilazimishe kuyafanya ili
kukifanya kipaji chako kidumu na kilete matokeo.
Ukiwa na kipaji na ukaishi maisha yasiyo na nidhamu uwe na uhakika kipaji chako
hakitaleta matokeo, kitaleta matokeo kidogo, ama kitaleta matokeo kidogo sana
au hakitadumu muda mrefu.
Kama unataka Kujifunza Zaidi Mbinu Za JINSI Ya Kukigeuza KIPAJI Kuwa PESA ”
Nashauri Usome nenda MediaForumz.blogspot.com
NO:
+255745228862 WhatsApp (Gadafi Nguile)
No comments:
Post a Comment